Habari za Tanzania

Editorial

Like Our Page

LULU APORA BWANA WA MTU

LIZABETH Michael ‘Lulu’ anayetesa katika filamu za Kibongo, yupo kwenye bifu zito na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid ambaye anadai amempora bwana’ke.
Staa Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika pozi.
Habari zinaeleza bifu lao limefikia hatua ya kuanikana waziwazi hadi kumwagiana matusi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram lakini huondoa majibizano yao machafu kila baada ya muda mfupi.
Chanzo cha habari hizi kinapasha kuwa ugomvi wa Lulu na Husna ni juu ya mwanaume huyo ambaye anaishi jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Seki anayeelezwa kuwa na pesa za kutosha kusumbua mjini. “Hao wanamgombea jamaa fulani wa Arusha, anaitwa Seki, ana mawe (pesa) mbaya.
Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2012, Husna Maulid.
Lakini wa kwanza kuwa na Seki ni Husna na Lulu alijua, sema Husna na huyo jamaa walikuwa wanagombana na kumwagana mara kwa mara. Sijui sasa nini kilimfanya Lulu kwenda kutembea tena na huyo jamaa wakati anajua ni wa shoga yake, labda ni baada ya kujua wamemwagana,” kilipasha chanzo hicho.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Baada ya kupata habari hizi, mwandishi wetu aliwatafuta Lulu na Husna kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo. Lulu alikuwa wa kwanza kupatikana ambapo alisema: “Jamani mimi simjui kabisa Husna Maulid wala hata katika fikra zangu hayupo... yaani kifupi simjui.”
Husna alipopatikana na kuelezwa mkanda mzima, kwanza alishangaa Lulu kutomjua, akasema: “Hakuna mtu asiyejua kuwa Lulu kanipora mwanaume wangu. Lakini anajifanya mjanja, tutaoneshana tu. Anajidai sana, anajifanya wa mjini hanijui mimi, lakini mimi ni wa mjini zaidi yake.”

Tags:

Related Posts

No comments:

Leave a Reply

HABARI KALI ZAIDI

Blogs Rafiki

Scroll to top